Skip to main content

KURA YETU, KIBOKO YAO


Wakati ni sasa kwetu si wakenya
Kuwafunza wanasiasa kuwa tumeshamanya
Hila zao za ufala hawataweza kutukanganya
Kura yetu ndio kiboko yao.

Juzi wasubiri usiku ati kujipa mamilioni
"Leo nawaita mafi ya kuku mnafikiria hatuoni"
Ufisadi mwafanya usiku wakenya wafa hospitalini
Kura yetu ndio kiboko yao

Nawaambia ukweli hawa nyie wabunge mafidhuli
Tumeishaipata yenu dawa fedha zetu tena hamli
Tunawachukia kama chawa hatuwapi tena shughuli
Kura ndio kiboko yao.

Nawasihi wote wakenya tujitokeze kwa wingi
Tariki ni nne machi tuwaonyeshe mwenye nguvu
Kwa umoja na udugu tutende haki yetu
Kura yetu ndio kiboko yao.


Comments

Popular posts from this blog

Umuhimu wa kiswahili

Kiswahili ni mojawapo wa lugha za kiafrika ambayo inakua kwa kasi mno. Katika Afrika ya mashariki kiiswahili knazungumzwa kati nchi za Kenya, Tanzania ,Uganda, Rwanda na Burundi. Aidha kiswahili kinazungumzwa katika nchi za Congo na Zaire. Hapa nchini kenya na Tanzania kiswahili kimefanywa kuwa lugha rasmi hali kadhalika lugha ya taifa. kiswahili pia kimefanywa kuwa lugha rasmi katika kongamano zote za Umajo wa Afrika yaaani African Union.  Hivyo basi tukizingatia haya hatuna budi kusema ya kwamba nafasi na manufaa ya kiswahili katika lugha ya kiswahili ni chungu nzima. Katika makala haya yetu tutazidi kuangazia lugha ya kiswahili kama kigezo cha undeleshaji wa uchumi barani Afrika na ulimwenguni kote kwa ujumla.

Mambo Ya Badilika:

Tariki yenyewe nane nane ,  imewadia Wakati sasa ni wetu, wananchi kujitetea Hakikisha kura umepiga kwa asiye na doa Haijalishi NASA au Jubilee mambo yabadilika Siasa duni za ufidhuli kataa katakata Walowezi na wafisadi tupa kama taka Kamwe hatutaki damu tena kumwagika Haijalishi NASA au Jubilee mambo yabadilika Wito natoa, kwetu sisi vijana Kesho hatofika, uongozi tungechukua jana Wazee twawaeleza na tena kwa bayana Haijalishi NASA au Jubilee mambo yabadilika Mamlaka msipo tupa hatuna budi kuyanyakua   Miaka mingi ya ujana tumepoteza kiholela Kwa kutumiwa vibaya na wakorofi wanasiasa Haijalishi NASA au Jubilee mambo yabadilika