Skip to main content

Mambo Ya Badilika:

Tariki yenyewe nane nane,  imewadia
Wakati sasa ni wetu, wananchi kujitetea
Hakikisha kura umepiga kwa asiye na doa
Haijalishi NASA au Jubilee mambo yabadilika

Siasa duni za ufidhuli kataa katakata
Walowezi na wafisadi tupa kama taka
Kamwe hatutaki damu tena kumwagika
Haijalishi NASA au Jubilee mambo yabadilika

Wito natoa, kwetu sisi vijana
Kesho hatofika, uongozi tungechukua jana
Wazee twawaeleza na tena kwa bayana
Haijalishi NASA au Jubilee mambo yabadilika

Mamlaka msipo tupa hatuna budi kuyanyakua  
Miaka mingi ya ujana tumepoteza kiholela
Kwa kutumiwa vibaya na wakorofi wanasiasa
Haijalishi NASA au Jubilee mambo yabadilika

Comments