Skype Language Classes - Find Language Tutors all over the World!: Tutors for Kiswahili : KENYA Daniel Native language: Kiswahili I speak: Kiswahili, Kamba, English US$ 35 per 30-minute lesson US$ 45 per 45-minute le...
Wakati ni sasa kwetu si wakenya Kuwafunza wanasiasa kuwa tumeshamanya Hila zao za ufala hawataweza kutukanganya Kura yetu ndio kiboko yao. Juzi wasubiri usiku ati kujipa mamilioni "Leo nawaita mafi ya kuku mnafikiria hatuoni" Ufisadi mwafanya usiku wakenya wafa hospitalini Kura yetu ndio kiboko yao Nawaambia ukweli hawa nyie wabunge mafidhuli Tumeishaipata yenu dawa fedha zetu tena hamli Tunawachukia kama chawa hatuwapi tena shughuli Kura ndio kiboko yao. Nawasihi wote wakenya tujitokeze kwa wingi Tariki ni nne machi tuwaonyeshe mwenye nguvu Kwa umoja na udugu tutende haki yetu Kura yetu ndio kiboko yao.