Ubeti wa kwanza natoa wito Kwa wakenya wapendwa Lugha ndiyo kiini cha mazungumzo Huleta watu pamoja Huwa kiwakilishi cha jamii Kiswahili lugha ya taifa Kinatumika hata ughaibuni Wenyaji twakipuuza Tukienzi kiingereza Ukoloni mamboleo Kila siku twaendeleza Kiaswahili twakidhihaki Utamaduni wetu twautupa Mwacha mila ni mtumwa Ndio maana twaangaika Hatujui lipi la kufuata Uingereza ama Marekani Nawasihi wapendwa Fikra tuzindue Tufuate yetu Waafrika Tujiendeleze ipasavyo Kiswahili tukikuze Tujivunie lugha yetu