Tariki yenyewe nane nane , imewadia Wakati sasa ni wetu, wananchi kujitetea Hakikisha kura umepiga kwa asiye na doa Haijalishi NASA au Jubilee mambo yabadilika Siasa duni za ufidhuli kataa katakata Walowezi na wafisadi tupa kama taka Kamwe hatutaki damu tena kumwagika Haijalishi NASA au Jubilee mambo yabadilika Wito natoa, kwetu sisi vijana Kesho hatofika, uongozi tungechukua jana Wazee twawaeleza na tena kwa bayana Haijalishi NASA au Jubilee mambo yabadilika Mamlaka msipo tupa hatuna budi kuyanyakua Miaka mingi ya ujana tumepoteza kiholela Kwa kutumiwa vibaya na wakorofi wanasiasa Haijalishi NASA au Jubilee mambo yabadilika
Skype Language Classes - Find Language Tutors all over the World!: Tutors for Kiswahili : KENYA Daniel Native language: Kiswahili I speak: Kiswahili, Kamba, English US$ 35 per 30-minute lesson US$ 45 per 45-minute le...